Charity Club cha Madereva Watembelea Kituo cha Watoto Yatima

Chama cha Charity (chariy club)cha madereva wa Shule ya Awali na Msingi Fountain Gate Dodoma kupitia Fountain Gate Foundation mapema leo wametembelea kitio cha kulea watoto yatima cha Tupendane kilichopo Kikuyu jijini Dodoma lengo likiwa ni kupeleka chochote walichonacho ikiwa ni sehemu ya kupongeza jitihada za kituo hicho kuelekea likizo ya kumaliza Muhula wa kwanza wa masomo 2023.

Pamoja nao
wameambatana na viongozi wa Foutain Gate Foundation akiwemo Meneja wake Denis Joel.

Taasisi ya Fountain Gate Foundation imetoa shukurani kwa Umoja wa madereva wa Shule ya Awali na Msingi Fountain Gate Dodoma kwa ajili ya kuikumbuka jamii inayotuzunguka.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*