Foundation Yaitembelea Kituo Cha Binti Shamsi

Taasisi ya Fountain Gate Foundation imeambatana na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Fountain Gate Dodoma imetembelea katika Kituo cha kulea Watoto yatima Bint Shamsi kilichopo maeneo ya Kisasa, Dodoma na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo Unga, Sabuni za kufulia na vinginevyo.

Umekuwa ni uataratibu wa kawaida wa Fountain Gate Foundation kutembelea katika vituo mbalimbali na kuwagusa Watoto wenye uhitaji ili kuwagusa Kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali.

Hatua ya Wanafunzi wa Fountain Gate Dodoma kushiriki katika Shughuli hiyo ni jitihada za Shule katika kuhakikisha wanawafundisha Watoto matendo ya huruma.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*