FOUNTAIN GATE FOUNDATION WAELEZEA FURSA KUSOMA NJE YA NCHI

FOUNTAIN GATE FOUNDATION WAELEZEA FURSA KUSOMA NJE YA NCHI

Muelimisha Rika kutoka Fountain Gate Foundation Cherry Makau amewaambia Wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Fountain Gate Dodoma Kuna faida nyingi sana za kusoma nje ya nchi.

Akizungumza na Wanafunzi hao amewaambia kuwa inasaidia kuongeza uelewa wa vitu mbalimbali, lakini pia inasaidia kujifunza mambo na Tamaduni Mpya japo amewasihi kufuata Yale yaliyo chanya tu.

Amezungumza hayo akiwaambia kuwa Taasisi inatoa nafasi Kwa Wanafunzi kuweza kuendelea na Masomo yao nje ya nchi, lakini amewakumbusha kuwa Nidhamu itabaki kuwa kitu muhimu kupata nafasi hizo.

Kwa hatua nyingine amewaambia kwamba Vipaji ni miongoni kwa vipaumbele kwa Wanafunzi kupata nafasi ya wao kwenda nje Kwa ajili ya Masomo. Hivyo wanatakiwa kuendelea kukuza vipaji kwani vitawasaidia siku zijazo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*